Swali: al-Qardhwaawiy anasema kuwa inajuzu kwa wanaume na wanawake kucheza filamu za maigizo. Ametumia dalili ya visa vilivyokuja katika Qur-aan na kusema kuwa Qur-aan inaegemea katika usulubu wa burudani. Ametaja visa vingine kutolea mfano kama vile kisa cha Sulaymaan (´alayhis-Salaam) na wadudu chungu na ndege, watoto wa Aadam na kunguru na Ismaa´iyl (alayahis-Salaam). Kisha akasema:

“Haiingii akili tukaharamisha picha, maigizo au kitu kingine katika mahitaji ya leo.”

Vipi tutamraddi al-Qardhwaawiy kwa aliyoyasema?

Jibu: al-Qardhwaawiy hastahiki kingine isipokuwa kipigo kama ambacho ´Umar alimpiga Swabiygh ili mabalaa yatoke kichwani mwake. Kutumia kwake dalili Qur-aan ya kwamba maigizo yanajuzu amemnasibishia uongo Allaah na Qur-aan. Mwenye kumzulia Allaah na Qur-aan uongo ni mwongo mzushi. Lau kama nisingemchukulia kuwa anayafasiri mambo kimakosa basi ningemkufurisha.

Kuhusiana na picha, mimi – na himdi zote ni za Allaah – nimeandika kitabu kilichochapishwa kwa jina “Hukm Taswiyr Dhaat-il-Arwaah”. Kinauzwa madukani.

Kuhusu hukumu ya kucheza maigizo, rejea katika kitabu kilichoandika Shaykh Bakr Abu Zayd. Kinatosha!

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 76
  • Imechapishwa: 08/10/2016