Swali: al-Qardhwaawiy anasema katika kitabu “al-Halaal wal-Haraam”, uk. 470, kama alivyotajwa katika Radd ya Shaykh al-Fawzaan, kwamba imewekwa katika Shari´ah kuwapenda mayahudi na wakristo na kuishi nao vizuri, kwa utulivu na kuwapenda. Hatimaye akasapoti fikira hii, ambayo ni kuwapenda mayahudi na manaswara, akataja shubuha nyingi. Tunataka kutoka kwa Shaykh wetu aziraddi. Utata wa kwanza ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

”Allaah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu – hakika Allaah anapenda wafanyao uadilifu. Hakika si vyengine Allaah anakukatazeni juu ya wale waliokupigeni vita katika dini na wakakutoeni kutoka majumbani mwenu na wakasaidiana juu ya kukutoeni [ndio anaokukatazeni] kufanya urafiki nao. Na yeyote atakayewafanya marafiki basi hao ndio madhalimu!” 60:08-09

Anasema kuwa Aayah hizi mbili ni zenye kuenea zinaonyesha namna matangamano yetu yanavyotakiwa kuwa kwa mayahudi na manaswara.

Jibu: Aayah hii inafanana na Hadiyth ya mama yake Asmaa´ bint Abiy Bakr (Radhiya Allaahu ´anhaa) alipokuja al-Madiynah ilihali alikuwa ni mshirikina. Akataka kumpa Asmaa´ zawadi. Asmaa´ akamuomba idhini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akawa amempa idhini. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anasema kuhusiana na mafungamano na wazazi wawili:

وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا

“Lakini wakikufanyia juhudi kwamba unishirikishe na yale usiyokuwa na elimu kwayo, basi usiwatii. Suhubiana nao kwa wema duniani.” 31:15

Mambo yakishakuwa hivo, kuna Aayah nyingi zinazotukataza kuwapenda:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi vyenu ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya imani; na yeyote katika nyinyi atakayewafanya wapenzi basi hao ndio madhalimu.” 09:23

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ

“Hutowapata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho wanafanya urafiki na wale wanaopingana na Allaah na Mtume Wake – japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao au jamaa zao.” 58:22

Je, maadui wa waislamu hii leo ni wenye kuwapa amani waislamu? Au wao wanachotaka ni kuutokomeza Uislamu na waislamu? Wameusaga Uislamu Andalusia na Ufilipino na wamekata matiti ya mwanamke wa Kiislamu. Hali kadhalika Bosnia na Herzegovina. Wamevamia Uislamu ndani ya miji ya Kiislamu. Kuna serikali nyingi zisizowaacha wanachuoni kufanya uwajibu wao. Wamesalitiwa na maadui wa waislamu. Wanaogopa Da´wah. Wanauogopa Uislamu wa kweli. Hivi sasa wanazingatiwa kuwa ni makafiri wenye kupigwa vita, Harbiyyuun, kwa kuwa wameivamia miji ya Kiislamu na kutunga kanuni katika miji ya waislamu. Wanazingatiwa kuwa ni makafiri wa kupigwa vita. Kwa msemo mwingine hawana amani yoyote kwa waislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 32-34
  • Imechapishwa: 08/10/2016