Swali: al-Qardhwaawiy ametaja baadhi ya Aayah zinazokataza kuwapenda makafiri kama mfano wa:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“Enyi walioamini! Msifanye mayahudi na manaswara marafiki vipenzi. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.” 05:51

Kisha akasema kuwa Aayah hizo zimekuja kuwahusu wale makafiri wanaowapiga vita waislamu. Katika hali hii haifai kwa waislamu kuwanusuru na kuwasapoti. Hii ndio maana ya mapenzi yaliyokatazwa. Kuwafanya marafiki kunapelekea kufichua siri za waislamu na kufungamana kunategemea na mkusanyiko na dini ya mtu alionayo.

Je, ni kweli Aayah hizi zinazokataza kuwapenda makafiri zinawahusu tu wale wenye uadui na wenye kuupiga vita Uislamu au ni zenye kuenea?

Jibu: Udhahiri wa Aayah ni zenye kuenea. Aayah zinazoonyesha njama zao dhidi ya Uislamu na waislamu:

وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ

“Hawatoridhika nawe mayahudi wala manaswaara mpaka ufuate mila zao.” 02:120

Matendo yao hii leo yanaonyesha kuwa hawako radhi na yeyote mpaka awe mnaswara. Inasikitisha, inasikitisha, inasikitisha kuna mtu anayedai kuwa ni mjuzi bingwa wa mambo ya kisasa ilihali ndiye mjinga wa mambo ya kisasa!

Ukimuuliza bibi kikongwe hapa Dammaaj ambaye hajui kusoma wala kuandika kuhusu mayahudi na wakristo, atasema kuwa ni maadui wa Allaah. Sembuze bibi kikongwe wa Palestina anayeona mayahudi wanavyowafanya. Sembuse bibi kikongwe wa Bosnia na Herzegovina. Kikongwe ni mjuzi zaidi kuliko Muftiy wa Qatar!

Muftiy wa Qatar ni mjinga kuliko punda. Kuna mtu asiyejua mashambulizi ya maadui wa Uislamu dhidi ya waislamu na Uislamu? Nasema hivo hata kama amehifadhi Qur-aan. Allaah amethibitisha ujinga kwa yule asiyetendea kazi elimu yake:

وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ

“Hakika walijua kwamba atakayeununua hatopata Aakhirah fungu lolote. Ni ubaya ulioje walichouzia kwayo nafsi zao – lau wangelikuwa wanajua!” 02:102

Mwanzoni amethibitisha elimu yao na mwishoni akaikanusha. Kwa kuwa yule asiyetendea kazi elimu yake anazingatiwa kuwa ni mjinga.

Nataraji kuwa mahakama ya Qatar itamtimua na kuleta Muftiy kutoka Saudi Arabia au mwanachuoni mwingine muheshimiwa. Qatar ni moja katika serikali bora. Wasiichafue nchi yao kwa mwendawazimu!

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 38-40
  • Imechapishwa: 08/10/2016