al-Qaradhwaawiy kuhusu jela ya mwanamke nyumbani

Swali: al-Qardhwaawiy anasema kuwa mwanamke kufungiwa nyumbani ni jambo halikujulikana isipokuwa katika kipindi ambacho ilikuwa kumuadhibu kwa sababu ya uzinzi na ilikuwa kabla ya kutimia Shari´ah halafu likafutwa:

وَاللَّاتِي يَأْتِينَ الْفَاحِشَةَ مِن نِّسَائِكُمْ فَاسْتَشْهِدُوا عَلَيْهِنَّ أَرْبَعَةً مِّنكُمْ ۖ فَإِن شَهِدُوا فَأَمْسِكُوهُنَّ فِي الْبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّاهُنَّ الْمَوْتُ أَوْ يَجْعَلَ اللَّـهُ لَهُنَّ سَبِيلًا

“Wale wanaofanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, basi washuhudisheni wanne kati yenu [walioona kitendo hicho], na wakishuhudia [kwamba wamekiona], basi wazuieni majumbani mpaka mauti yawafishe au Allaah awajaalie njia.” 04:15

Ni vipi kubaki nyumbani daima itakuwa ni sifa ya mwanamke katika maisha ya kawaida?

Jibu: Sio mfungwa. Ni mtwaharifu. Anatakiwa kusaidiwa katika utwaharifu wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaadamu ameandikiwa sehemu ya uzinzi na hakuna namna ya kuiepuka. Uzinzi wa macho ni kuangalia. Uzinzi wa masikio ni kusikia. Uzinzi wa ulimi ni maneno. Uzinzi wa mkono ni kushika. Uzinzi wa miguu ni kutembea. Moyo unaingiwa na matamanio na kutamani na tupu ima inathibitisha au inakadhibisha.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Katika matamshi ya Ibn Khuzaymah imekuja:

“Hata hivyo nyumba zao ni bora kwao.”

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anjashah! Kuwa na upole na glasi!”

Mwanamke ni kama glasi. Kwa hiyo anatakiwa kuangaliwa vizuri asije kupasuka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sijaona walio na akili punguani na dini pungufu wanaomghalibu mwanaume mwenye busara kama nyinyi [wanawake].”

Ameipokewa al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: skaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 56-57
  • Imechapishwa: 08/10/2016