al-Qaradhwaawiy kuhusu Aayah inayowaamrisha wanawake kutulizana majumbani

Swali: al-Qardhwaawiy anasema kuwa wanachuoni wanaokataza mwanamke kupiga kura wanatumia dalili maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ

“Na tulizaneni majumbani mwenu.” 33:33

al-Qardhwaawiy amejaribu kupingana na dalili hii kwa njia tano. Zimetajwa kwenye gazeti la “ad-Da´wah”[1]. Moja katika njia hizo ni kwamba Aayah inawahusu wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yao.

Jibu: Aayah inawazungumzisha wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mwishoni wake inawahusu wanawake wote, kama alivyosema Shaykh Muhammad al-Amiyn ash-Shanqitwiy katika “Adhwaa´-ul-Bayaan”.

Dalili ni ya jumla na inawahusu wanawake wote midhali mtu hakudharurika kutoka kama vile mjane na wengineo. Allaah (´Azza wa Jall) anasema:

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا

“Na waambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yenye kudhihiri.” 24:31

Hata kama inawazungumzisha wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ueneaji uliyokuja katika Aayah hii unafahamisha kuwa ni wanawake wote.

[1] Nambari. 65. 1418/2005.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: skaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 51.52
  • Imechapishwa: 08/10/2016