al-Qardhwaawiy anawaita wanawake wa Kiislamu kupiga kura na wawe ni mfano wa Answaar wa leo


Swali: al-Qardhwaawiy anasema ya kwamba kuna haja wanawake wenye msimamo waingie katika vituo vya kupiga kura ili wapige kura na wakabiliane na wanawake wa kisekula wanaosema wanaongoza wanawake wa ulimwenguni. Haja ya kijamii na ya kisiasa inaweza kuwa kubwa na muhimu zaidi kuliko haja ya binafsi inayomruhusu mwanamke kutoka [nyumbani] kwa ajili ya maisha yake ya kawaida.

Jibu: Sijui hata niseme nini. Mtu anakaribia kuyatapikia maneno yake haya yaliyooza. Umekhasirika na kuangamia. Hivi kweli unawaita wanawake wa Kiislamu kutoka majumbani mwao kwa ajili ya kuinusuru Twaaghuut! Mambo haya ya uchaguzi tumeyatoa wapi? Kutoka kwa maadui wa kiislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kweli pale aliposema:

“Hakika mtafuata nyayo za wale walioishi kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika wakiingia katika shimo la kenge na nyinyi mtaingia pia.”

Kumraddi al-Qardhwaawiy ni bora kuliko ´ibaadah za Sunnah, swawm za Sunnah na swalah za Sunnah. Udanganyifu wa Ibliys! Mimi sintotaja Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili iafikiane na maneno haya ya kipumbavu, isipokuwa nitaitaja kwa ajili ya kutahadharisha wanachuoni waovu:

“Kikubwa ninachokhofia katika Ummah wangu ni mnafiki hodari wa kuzungumza.”

“Kikubwa ninachokikhofia katika Ummah wangu ni viongozi wenye kupotosha.”

Hivi kweli inajuzu kwa muislamu kumtetea mtu kama huyu?

Tunawaita wanachuoni wetu kusoma vitabu vyake vilivyofutwa kisha waviraddi. Tunawaita wanachuoni wetu waheshimiwa ambao tunawapenda kwa ajili ya Allaah. Wao ndio wanusuraji wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunawaomba wamraddi. Kama mfano wa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, Shaykh Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, Shaykh Rabiy´ [bin Haadiy al-Madkhaliy] na Shaykh Swaalih al-Fawzaan ambaye yeye ameshamraddi kuhusu kitabu chake “al-Halaal wal-Haraam”. Allaah amjaze kheri.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: skaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 08/10/2016