Tumezungumzia chuo kikuu cha al-Iymaan katika mikanda mitatu. Baada ya kumraddi al-Qardhwaawiy – Allaah akitaka – tutamraddi mtu wa khatari katika al-Ikhwaan al-Muslimuun. Anaitwa Swalaah as-Saawiy. Yeye na wale wanaomleta Yemen wanatakiwa kuwa katika hali ya kuchunga na wasubiri mkanda mmoja au mingi kwa kichwa cha khabari:

“al-Kaawiy li Dimaagh Swalaah as-Saawiy.”

Ni mwanaume wa khatari.

Kuhusu huyu al-Qardhwaawiy, anazumgumza maneno yanayomfurahisha mkanamungu, zandiki, myahudi na mnaswara ilihali waislamu ndio wanazidi kumchukia tu. Kuna watu wanaokereka kwa kuenezwa na kutetewa Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawako tu tayari kuitetea batili.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 27
  • Imechapishwa: 08/10/2016