al-Qaradhwaawiy anaufedhesha Uislamu

Swali: al-Qardhwaawiy aliulizwa kuhusu msimamo wa Uislamu juu ya magharibi na kama kuna uwezekano magharibi na Uislamu vikakurubiana. Nidipo al-Qardhwaawiy akajibu ya kwamba sisi tumeamrishwa kujadiliana na wamagharibi hawa na kuongea nao kwa njia iliokuwa nzuri. Anayesoma Qur-aan ataona jinsi inavyochukua msitari wa mbele kabisa katika kujadili kwa njia nzuri. Mitume walijadiliana na watu wao kama ilivyorekodiwa katika Qur-aan. al-Qardhwaawiy akataja mjadala wa Nuuh na watu wake, mjadala wa Ibraahiym na watu wake na baba yake na mjadala wa Muusa na Fir´awn. Baada ya hapo akatilia nguvu kushangazwa kwake na akasema namna Allaah alivyojadiliana na Ibliys:

قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ ۖ أَسْتَكْبَرْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ الْعَالِينَ

“Akasema: “Ee Ibliys! Ni kipi kilichokuzuia usimsujudie yule Niliyemuumba kwa Mikono Yangu? Je, umetakabari au umekuwa miongoni mwa waliojitukuza?”” 38:75

Anasema kuwa haya yanafahamisha kuwa Uislamu unakaribisha mdahalo na kwamba Qur-aan, Sunnah na mirathi ya Kiislamu imejaa midahalo hii. al-Qardhwaawiy anasema kuwa yeye ni mmoja miongoni mwa wale wanaoita katika midahalo hii. Anasema katika kitabu “al-Islaam wal-Gharb”, uk. 86:

“Katika sifa ya mjadala huu tunaoita ni kwamba tunajadili na kila mmoja ashikamane na mfumo wake.”

Tazama vilevile ukurasa wa 18 na 58.

Jibu: Vitabu vyako vya kwanza havikufanikiwa, wewe al-Qardhwaawiy. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) alisema kumwambia Ibliys:

قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِي إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ

“Akasema: “Basi toka humo, kwani hakika wewe umefukuzwa. Hakika laana Yangu iko juu yako mpaka Siku ya malipo.”” 38:77-78

Mijadala na maadui wa Uislamu inafanywa na wanachuoni wanaoupa Uislamu hadhi na wanajitukuza kwa Uislamu. Haifanywi na wakhasirikaji wanafagilia ustaarabu wa Ulaya. Watu kama hao wanauweka Uislamu katika udhalilisho na utwevu. Mijadala kama hii inatakiwa kufanywa na wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah kama vile Shaykh Ibn Baaz, Shaykh al-Albaaniy na mfano wao.

Kuhusu wewe, umejulikana msimamo wako. Umeanguka. Hatukuamini. Namshukuru Allaah kuona vijana wamekupa mgongo wewe, vitabu vyako na Da´wah yako. Huenda umefikia miaka sabini au kitu kama hicho. Kilicho bora kwako ni wewe kujitenga na ubaki nyumbani kwako mpaka pale shaytwaan atapotoka kichwani mwako. Pale ambapo shaytwaan anayekutia wasiwasi kichwani mwako atapotoka ndipo unaweza tena kurudi kutangamana na waislamu na kukaa nao. Unahitajia mtu wa kukutibu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: skaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 40-42
  • Imechapishwa: 08/10/2016