al-Qardhwaawiy anaonelea kuwepo kwa makundi mengi ni jambo zuri

al-Qardhwaawiy anasema katika baadhi ya vitabu vyake kwamba kuwepo kwa makundi mengi ya Kiislamu ni jambo linafahamisha usalama wa Uislamu. Usalama? Iko wapi dalili juu ya hayo unayoyasema? Marekani na maadui wa Uislamu ndio wenye kupanga vijikundikundi. Wasingelikuwa na maslahi kwa hayo basi wasingetusaidia. Wanatoa mamilioni ya dola wakati wa uchaguzi.

Mwandishi wa “Fiqh-uz-Zakaah”! Nakupa changamoto uniletee dalili moja tu yenye kuruhusu makundi mengi. Ama kuhusu sisi, sikiliza! Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika mkono wa Allaah uko pamoja na mkusanyiko.”

Hakusema:

Hakika mkono wa Allaah uko pamoja na mikusanyiko.”

“Mwenye kuacha mkusanyiko kiasi cha shibri na akafa, basi amekufa kifo cha kipindi cha kishirikina.”

Hakusema:

“Mwenye kuacha mikusanyiko kiasi cha shibri na akafa, basi amekufa kifo cha kipindi cha kishirikina.”

Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) alisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Vipi kusipokuwepo mtawala wala mkusanyiko?” Hakusema: “Vipi kusipokuwepo mtawala wala mikusanyiko?”

Nipe Hadiyth moja tu inayotaja makundi mengi. Bali Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane.” 03:103

إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ

“Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundi makundi, huna lolote kuhusiana nao.” 06:159

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

”Hii njia Yangu, [njia] iliyonyooka; basi ifuateni na wala msifuate vichochoro [vingine] vikakufarikisheni na njia Yake!” Hivyo ndivyo alivyokuusieni kwayo; ili mpate kumcha.” 06:153

وَإِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ

”Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja Nami ni Mola wenu. Hivyo nicheni.” 23:52

Ni wajibu kwa waislamu wawe na umoja:

“Muislamu kwa muislamu mwenzake ni kama majengo; upande mmoja unaupa nguvu mwingine.”

“Mfano wa waislamu katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kufanyiana upole ni kama mwili mmoja; kiungo kimoja kinapopatwa na maumivu basi mwili mzima unapatwa na maumivu na homa.”

Ni wajibu, wajibu, wajibu kwa Yuusuf al-Qardhwaawiy kupigiwa marufuku kuzungumza mpaka kwanza apimwe na daktari wa akili. Kuna khatari kuwa maadui wa Kiislamu wamemuosha kichwa chake na akawa kama mwendawazimu. Vilevile mfano wa al-Qardhwaawi, kama az-Zindaaniy, ni lazima kuwapigia marufuku.

Ahl-us-Sunnah! Ni wajibu kwenu kumshukuru Allaah (´Azza wa Jall). Watu wamejua nyinyi ni kina nani. Wanajua kuwa ni wakweli. Wameijua Da´wah yenu. Wamejua Ikhlaasw yenu na kwamba mnalingania katika dini ya Allaah pasi na kutaka kutoka kwa yeyote malipo wala shukurani. Ni wajibu kwenu kumhimidi Allaah. Ni wajibu kwenu kuipa nyongo dunia kikweli.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 08/10/2016