al-Masiyh ad-Dajjaal atatoka kabla ya dunia kwisha au baada yake?

Swali: Je, al-Masiyh ad-Dajjaal atatoka baada ya watu kufufuliwa au kabla ya hapo?

Jibu: al-Masiyh ad-Dajjaal atatumwa mwishoni mwa dunia kabla ya watu kufufuliwa. Baada ya kufufuliwa hakuna jengine isipokuwa kusimama mbele ya Allaah kwa ajili ya hesabu. Miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah ni kwamba atajitokeza kiumbe katika wana wa Aadam na atatoka katika zama za mwisho ambaye kwanza atadai kuwa ni mwema, kisha baada ya hapo adai utume halafu baada ya hapo adai uungu. Atakuwa na mambo yasiyokuwa ya kawaida; kwa mfano atakuwa na pepo na moto, atakuwa na uwezo wa kumuua mtu kisha Allaah anamuhuisha, siku ya kwanza ya ad-Dajjaal urefu wake utakuwa kama urefu wa mwaka, siku yake ya pili itakuwa kama mwezi, siku yake ya tatu itakuwa kama wiki, kama ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh. Imekuja katika “as-Swahiyh” ya Muslim Hadiyth ikiwa na maana ifuatayo:

“Tangu aumbwe Aadam mpaka kusimame Saa hakujapatapo kuwepo kwa jambo kubwa kama ad-Dajjaal.”

Au Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema maneno mfano wa hayo.

Kwa ajili hii ndio maana tumewekewa katika Shar´ah tujilinda kutokamana na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal mwishoni mwa swalah katika Tashahhud.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 07/03/2018