Swali 224: Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy aliulizwa na baadhi ya watu wa Algeria swali lifuatalo:

Muulizaji: Shaykh wetu! Imetufikia khabari kwamba wewe ni miongoni mwa waliobeba bendera ya al-Jarh wa Ta´diyl katika zama hizi. Tunapendelea kukuuliza juu ya baadhi ya watu ambao wana nafasi hapa kuhusu baadhi ya wapambanaji. Tunaanza na Abu Qataadah al-Falastwiyniy ambaye anaishi Uingereza. Je, unamjua?

Shaykh: Nasikia kuwa mtu huyu ni miongoni mwa viumbe waovu na mwenye matendo machafu kabisa juu ya fatwa na kwamba anahalalisha kuwaua watoto na wanawake. Ni uovu ulioje wa aliyoyafanya na ni uovu ulioje wa aliyoyafutu mtu huyu! Mtu huyu si katika wanachuoni. Huyu ni katika watu wenye kufuata matamanio. Miongoni mwa dalili ya hayo ni kwamba anaishi katika nchi ya kikafiri. Mimi nina wasiwasi kwamba Uingereza inawapa nguvu watu sampuli hii kwa sababu wanautakia Ummah wa Uislamu maangamivu. Watu hawa wameushusha Ummah wa Kiislamu kwenye maangamivu na uteketeaji, mambo ambayo yanawafurahisha makafiri. Matukio haya ambayo wamewafikia wa-Algeria ni kina nani wenye kufurahishwa nayo? Yanawafurahisha mayahudi, wakristo na maadui wa Uislamu. Ni yepi yaliyowafikisha raia wa-Algeria katika matukio haya yenye kutia uchungu kama si fatwa hizi? Je, mnamtambua Abu Qataadah kama Salafiy?

Muulizaji: Hatumtambui kama Salafiy.

Shaykh: Salafiy?

Muulizaji: Hatumtambui kama Salafiy.

Shaykh: Hatumtambui kama Salafiy. Ina maana ni Takfiyriy?

Mtu mmoja akasema: Naona kuwa ni Takfiyriy.

Mwingine aliyekuwa pale akaitikia: Ndio ni kweli.

Shaykh: Unamjua kisha unaniuliza mimi juu yake?

Muulizaji: Lengo nimetaka ndugu zangu wajue. Kwa sababu ndugu ni wenye kukosea juu yake. Wataposikia maneno yako na wewe unastahiki kumzungumzia basi watayachukua maneno yako – Allaah (´Azza wa Jall) akitaka.

Shaykh: Allaah akujaze kheri.

Muulizaji: Shaykh wetu! Unamjua Abu Musw´ab as-Suuriy?

Shaykh: Ni nani huyo Abu Musw´ab?

Muulizaji: Ni msiria.

Shaykh: Anaishi Uingereza?

Muulizaji: Huenda. Yeye pia anazungumzia masuala haya ya Takfiyr na Jihaad.

Shaykh: Abu Hamzah. Ni miongoni mwa viongozi wa shari na fitina. Nafikiri kuwa wana mafungamano na maadui wa Uislamu. Ni mamoja Uingereza au kwenginepo na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Wao ndio wenye kuwashaji´isha juu ya fitina hii wanayoichochea katika nchi za Kiislamu na juu ya fatwa hizi zinazowadhuru waislamu na wala haziwanufaishi.

Muulizaji: Shaykh wetu! Unasemaje juu ya Usaamah bin Laadin?

Shaykh: Ninaapa kwa Allaah kwamba hayuko mbali na watu hawa. Hayuko mbali na watu hawa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 465-466
  • Imechapishwa: 11/04/2020