al-Madkhaliy akimsifia adh-Dhwafayriy na kusema kwamba Salafiyyah yake ni yenye nguvu

Swali: Je, watu wachukue elimu kutoka kwao Mashaykh hao?

Jibu: Ndio. Elimu ichukuliwe kutoka kwa [… haisikiki vzr… ], Khaalid adh-Dhwafayriy na ´Aadil bin Mansuur. Hawa ni miongoni mwa walinganizi wanaolingania kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na ni miongoni mwa watu wenye Salafiyyah yenye nguvu kabisa. Wana uchangamfu na kuwashaji´isha Salafiyyuun katika miji ya kiarabu na miji mingine. Nawanasihi ndugu wachukue elimu kutoka kwao. Namnasihi yule anayewazungumza kwa ubaya auzuie mdomo wake. Kwani kufanya hivo ni katika kuzuia watu kutokamana na njia ya Allaah. Allaah awanufaishe wote katika yale anayoyapenda na kuyaridhia.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=EoGMmqdSvGA
  • Imechapishwa: 26/11/2019