Swali: Kwa nini leo kunazungumzwa sana juu ya kwamba Shaykh Rabiy´ ni Murjiy´ na haya na yale?

Jibu: Ni nani?

Swali: Shaykh wetu na ´Allaamah Rabiy´. Kwa nini leo anazungumziwa sana?

Jibu: Sikiliza! Sikiliza! Shaykh Rabiy´ ni neema ya mtu. Kuna kheri kwake. Kwa masikitiko makubwa vijana hawa wana ujasiri wa kujeruhi pasina elimu. Unasikia?

Muulizaji: Ndio.

al-Luhaydaan: Ni sababu inayoondosha baraka ya elimu.

Swali: Unamaanisha kuwa maneno ya watu hawa yasikubaliwe pasina kujali wanachosema?

Jibu: Kamwe. Yasikubaliwe. Yasikubaliwe.

Swali: Wanasema kuwa anawasema vibaya wanachuoni na anaraddi kila wakati.

Jibu: Hapana, hawasemi vibaya wanachuoni. Anawaraddi watu wenye kufanya madhambi hadharani na wanastahiki Radd.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=146268
  • Imechapishwa: 07/05/2018