al-Luhaydaan Kuhusu Matahadharisho Ya Shaykh Rabiy´ Kwa al-Hajuuriy


Swali: Je, yachukuliwe maneno ya Shaykh Rabiy´ bin Haadiy ´Umar al-Madkhaliy kutahadharisha kwake Shaykh Yahyaa al-Hajuuriy?
Jibu: Ikiwa anamkosoa mtu huyu sifikirii kuwa Shaykh Rabiy´ atamkosa mtu asiyemjua. Amefanya hivyo kwa sababu tu anamjua.

Swali: Kwa hiyo mtu anaweza kuchukua maneno ya Shaykh Rabiy´?

Jibu: Ninatumai hakuna neno – in shaa Allaah. Mimi simjui mtu huyu. Sijasoma kitu katika maneno yake ili niweze kujua na maoni yaliyojengeka juu ya ujuzi na elimu.

Swali: Shaykh Rabiy´ anasema kuwa amemnasihi mara nyingi lakini hataki kurudi katika haki. Amekuja na dalili.

Jibu: Tafuteni mtu mwengine. Achaneni naye. Elimu haikufungamana na mtu mmoja tu.

Swali: Je, ni sahihi kwa yule mwenye kumtetea? Katika hali hiyo anakuwa ni mtu gani?

Jibu: Hapana, usimtetee. Usimtetee mtu ambaye hujui anakosa kasoro.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=140436
  • Imechapishwa: 18/01/2017