al-Luhaydaan kuhusu al-Gharyaaniy na Rabiy´ al-Madkhaliy

Swali: Tumefikiwa na maneno ya Shaykh Rabiy´ (Hafidhwahu Allaah), Shaykh Muhammad bin Haadiy (Hafidhwahu Allaah) na Shaykh Ahmad Bazmuul (Hafidhwahu Allaah) kuhusu as-Swaaqid al-Gharyaaniy. Je, yachukuliwe maneno yao juu yake na wao ni katika wanachuoni…

Jibu: al-Gharayaaniy ambaye ni Muftiy wa Libya?

Muulizaji: Ndio.

al-Luhaydaan: Kwa kweli sijui chochote juu yake isipokuwa tu naona kuwa amekosea kuwalazimisha kufunga.

Muulizaji: Anasema pia kuwa ni lazima kwa waislamu wote kutoka nje na kuandamana…

al-Luhaydaan: Kwa hali yoyote ile ina maana kwamba anafuata mfumo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun.

Muulizaji: Ina maana kwamba yachukuliwe maneno ya Mashaykh hawa? Je, ni waaminifu kwa sababu wapo baadhi ya vijana…

al-Luhaydaan: Nasema kwa kukata kabisa kwamba Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy ni mtu mtakasifu katika dini yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://darulhadith.com/al-luhaydan-om-al-gharyani-och-rabi%c2%b4-al-madkhali/
  • Imechapishwa: 27/09/2020