al-Lajnah ad-Daaimah kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh na vitabu kama “Fadhwaail-ul-A´mal”

Swali: Shaykh Muhammad Zakariyyah [al-Kaandahlawiy] ni katika wanachuoni wanaojulikana India na Pakistan na khaswa kwa Jamaa´at-ut-Tabliygh. Ameandika vitabu vingi. Moja wapo ni kitabu “Fadhwaail-ul-A´mal”. Kitabu hichi kinasomwa katika mizunguko ya kielimu za kidini za Jamaa´at-ut-Tabliygh. Wanachama wa kundi hili kitabu hichi wanaonelea kama “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na vinginevyo. Nilikuwa pamoja nao hapo kabla. Katika kipindi ambapo nilikuwa nasoma kitabu hichi, nilikuta visa ambavyo nilikuwa na uzito kuvifahamu na kuviamini. Ndio maana ninatuma hili katika kamati ili mnitatulie tatizo langu. Moja katika visa vilivotajwa ni kisa cha Ahmad ar-Rifaa´iy wakati alipoandika:

“Baada ya kuhiji, alitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akasoma mashairi mbele ya kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ghafla ukatoka nje mkono wa kulia wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya kaburi na akaubusu.”

Imepokelewa na as-Suyuutwiy katika “al-Haawiy”. Ametaja kwamba Waislamu 90.000 walikuwepo hapo ikiwa ni pamoja na Shyakh ´Abdul-Qaadir al-Jaylaaniy. Kutokana na haya ninataka kuwauliza yafuatayo:

1- Je, kisa hichi ni kweli?

2- Ikiwa ni kweli, ninauliza kama inajuzu kuswali nyuma ya mtu ambaye anakisimulia na kukiamini? Je, inajuzu kwake kuongoza Swalah?

3- Je, inajuzu kusoma vitabu hivi katika mizunguko ya kielimu ya kidini Misikitini. Kitabu hichi kinasomwa katika Misikiti ya Jamaa´at-ut-Tabliygh Uingereza na kinajulikana pia hata Saudi Arabia na khaswa al-Madiynah kwa sababu mwandishi aliishi muda mrefu al-Madiynah.

Swali: Kisa hicho ni batili na hakina asli. Maiti hafanyi harakati, sawa ikiwa ni Mtume au asiyekuwa Mtume, kwa kunyoosha mkono wake au kwa njia nyingine. Si sahihi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinyoosha mkono wake kwa ar-Rifaa´iy au mtu mwingine. Ni mawazo tu na ufikiriaji usiokuwa na uhalisia. Haijuzu kukiamini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunyoosha mkono wake kwa Abu Bakr, ´Umar au mtu mwingine katika Maswahabah seuze tusiseme watu baada yao. Mtu asidanganyike kwamba as-Suyuutwiy ametaja haya katika kitabu chake “al-Haawiy”. Hutaja kila kitu katika vitabu vyake.

Haijuzu kuswali nyuma ya mtu anayeamini kisa hicho kwa sababu anaamini ukhurafi na ana ´Aqiydah mbovu.

Haijuzu kusoma vitabu kama “Fadhwaail-ul-A´maal” kwa sababu ya ukhurafi na uongo ulionao, sawa ikiwa hilo litafanywa Misikitini au sehemu nyinginezo. Kwa sababu vitabu hivi vinawapotosha watu na vinaeneza ukhurafi kati yao.

Fatwa ya al-Lajnah ad-Daaimah nambari. 21412

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd