al-Kahf katika swalah ya sunnah siku ya ijumaa

Swali: Inasihi kusoma Suurah “al-Kahf” katika swalah ya sunnah siku ya ijumaa au ni lazima kuisoma ndani ya msahafu?

Jibu: Kuisoma imependekezwa. Hadiyth zenye kuzungumzia hilo zina baadhi ya udhaifu. Lakini akiisoma katika swalah ya sunnah au akiisoma nje ya swalah kunatarajiwa juu yake thawabu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 11/05/2019