Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika ya Allaah ni mzuri na Anapenda vilivyo vizuri.”

Je, hili linathibitisha kwamba al-Jamiyl, aliye mzuri, ni moja katika Majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na inajuzu kwa mtu akaitwa ´Abdul-Jamiyl?

Jibu: Hapana. Sio jina, ni kwa njia ya maelezo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa Allaah ni mzuri na Anapenda vilivyo vizuri. Hili ni kwa njia ya kumweleza Allaah (´Azza wa Jall) na sio kwa njia ya jina.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331103.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015