Swali: Kuna mwalimu anayetufunza mada ya kidini. Tumefaidika sana kutoka kwake, lakini baadhi ya wanafunzi wenzangu wananitahadharisha naye kwa sababu eti ni Jaamiy. Hii ina maana kuwa mtu aache kufaidika kutoka kwake? Ni kina nani Jahmiyyah ambao wanawataja na kuwagusia?

Jibu: Sijui Jaamiyyah yoyote. Ni jina walilolizua wao wenyewe. Silijui. Ikiwa ni unasibisho wa ndugu yetu Muhamamd Amaan al-Jaamiy, basi mimi namjua. Ni mwanachuoni. Mlinganizi wa Allaah. Sijui kutoka kwake isipokuwa tu mwenye kufuata haki. Nina uzoefu tu mzuri kwake. Lakini mnajua kuwa kuna watu wenye kuzua majina bandia kwa sababu ya kuwakimbiza watu kutokamana na haki. Huyu hakuna mwengine anayemdhuru isipokuwa yeye mwenyewe. Dini ni yenye kunusuriwa. Watu wa dini ni wenye kunusuriwa. Yule mwenye kujitenga nao mbali au akawaponda hakuna mwengine anayemdhuru isipokuwa yeye mwenyewe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=YvFojqy9S5U
  • Imechapishwa: 12/02/2017