al-Ikhwaan Ndio Mama Na ISIS Na an-Nusrah Ndio Wana


Hali kadhalika unaweza kusema juu ya vifaranga vyote vya mama wa Khawaarij: al-Ikhwaan al-Muslimuun. Wao ndio jukwaa na mama wa makundi yote haya. Vifaranga hivi vinatoka kwao.

Wamoja katika wao ni mtandao wa Sayyid Qutwub kuanzia 1385/1965. Sayyid Qutwub na wafuasi wao ndio bidhaa zao.

Wengine ni Jamaa´at-ut-Takfiyr wal-Hijrah.

Tatu ni Jamaa´at-ut-Tawaqquf wat-Tabayyun.

Nne ni Jamaa´at-ul-Jihaad.

Tano ni al-Jamaa´ah al-Islaamiyyah.

Sita ni kundi la ´Abdur-Rahmaan na wafuasi wake.

Wote hawa ni vifaranga vyao na walikuwa hivo mpaka alipokuja mama mwingine; al-Qaa´idah. ISIS ni moja katika kizazi chao. ISIS ndio mwana mkubwa na mwenye nguvu zaidi uwanjani hii leo. Halafu anafuata an-Nusrah. Wote hawa ni vifaranga vya al-Qaa´idah.

Vijukuu vyote hivi vinatokamana na mtandao wa Hasan al-Bannaa al-Ikhwaan al-Muslimuun. Ni kama alivyosema Shaykh Haamid al-Faqiy (Rahimahu Allaah):

خوان المسلمين

“Wandanyifu wa waislamu.”

Wamemdanganya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na waislamu na hivi sasa mnaona matunda yake.

Hakuna mwanachuoni yoyote aliye na pote hili. Hali kadhalika mazalisho ya al-Ikhwaan al-Muslimuun yaliyotajwa na wao hawana. al-Ikhwaan al-Muslimuun wote ni Takfiyriyyuun. Pasi na uvuaji wowote. Lakini hata hivyo wanatofautiana. Huenda kuna ambaye ataona kuwa nimekosea, lakini wacha turejee katika vitabu vyao. Haya yamo ndani ya vitabu vyao. Wote ni wakafirishaji. Kuna ambao wanaonelea mtu afanye upinzani na Takfiyr wakati wengine wanaona mtu anatakiwa afanye uteuzi. Wanataka kuwa na wafuasi wengi ili wafanye shinikizo kwa watawala. Haya ndio tulionayo. Miaka miwili iliyopita wadanganyifu wa waislamu – خوان المسلمين – walifanya maandamano na wakaandamana hadi kwenye soko ya Maydaan na wakawatia watu khofu kwa kuonyesha kuwa ni wengi na wana nguvu. Namna hii ndivyo ilivyoanza mikakati ya Hasan al-Bannaa katika zama za pili baada ya kuwa ameshafichuliwa na kuuawa. Kukatoka kitabu “Du´aat laa Qudhwaat”[1] na wakaanza kufanya uteuzi kwa watu ili kwa njia hiyo waweze kuwafanyia shinikizo serikali ili wafikie malengo yao.

[1] Cha Hasan al-Hudhaybiy.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/12009 Tarehe 1436-10-30/2015-08-15
  • Imechapishwa: 06/11/2016