al-Halabiy akitetea rai ya Muhammad assaan kuhusu maandamano


Ajabu si kwake tena – yaani Muhammad Hassaan – ajabu ni kwa ´Aliy Hassan bin ´Abdil-Hamiyd [al-Halabiy] na ambao wako katika utata wake. Wanamsaidia, wanamtetea na kumtakasa na vitendo vyake. Kwa masikitiko makubwa kwa njia ya ujanja ujanja. Unamuona ´Aliy Hassan bin ´Abdil-Hamiyd akimuombea na kusema:

“Allaah Ampambe kwa Taqwa – yaani Muhammad Hassaan. Ni kosa ambalo hatulikubali wala hatuliridhii.”

Hakuja kwa neno hata hata moja la kumkataza. Huu ni mchezo na njia ya kuwadanganya watu. Kwanza anasema:

“Ni kosa ambalo hatulikubali na kuliridhia.”

Baada ya hapo anarejea na kumtetea na kumsifia msimamo wake kama huu. Bali kwa masikitiko makubwa, anakubali kuwa kitendo chake kimeegamia katika misingi ya kanuni za Kishari´ah. Naapa wallaahi kuwa huu ni mgongano. Allaah Humwacha mtu muongo maneno yake yakajigonga yenyewe kwa yenyewe. Baada ya hapo anamkataza yule anayemwongelea Muhammad Hassaan na mbinu zake mbaya za kumtetea. Wakati fulani analaumu kwa kuwa eti wanamtumia yeye – yaani Muhammad Hassaan. Ni kweli. Ikiwa wewe unamtetea basi wewe ni kama yeye, sawa ukubali hilo au ukatae. Hawa watu hawakutumia chochote. Bali wamehukumu maneno yako. Kuna faida gani yakusema kuwa eti hukubali kosa lake wala huliridhii, halafu unarejea baada ya hapo na kumtakasa? Hili tumelisoma na kuliona kwa macho yetu wenyewe. Ikiwa hali ni hio hawa watu hawakutumia maneno yako. Bali wamekuhukumu kwa maneno yako. Na maneno yako yanathibitisha ukweli wao. Na wewe kwa hilo unathibitisha bendi yako kwa mtu huyu, sawa ukubali hilo au ukatae. Hatujali kuridhia kwako wala kukubali, maadamu maneno yako yamesikika, yakasomwa na kusajiliwa. Hili ni katika kucheza kwa maneno. Na Muhammad Hassaan tumeona maneno yake na kuyasikia. Unasema:

“Anaechunguza tukio si kama yule mwenye kulieshi humo, na yule ambaye miguu yake iko kwenye moto si kama yule aliye na miguu yake ndani ya maji.”

Huku ni kusifia kosa la Muhammad Hassaan kwa kuwa miguu yake yeye iko ndani ya moto na si kama wengine ambao miguu yao iko ndani ya maji. Unasema:

“Kanuni za wanachuoni wakubwa na wenye Dini, kuzuia madhara kunatangulizwa juu ya kuleta manufaa.”

Na mimi nasema kanuni za wanachuoni wakubwa wa Dini khaswa katika masuala haya ni kama alivyosema Shayk-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

“Hakika wanachuoni, watu wa Dini na fadhila hawamuachii yeyote katika aliyokataza Allaah kumuasi mtawala na kuwafanyia ghushi na kuwafanyia Khuruuj vovyote. Imekatazwa. Kama inavyojulikana katika ada ya Ahl-us-Sunnah tangu mwanzo hadi sasa.”

Namwambia ndugu ´Aliy amche Allaah. Haya ndio wayasemwayo kwawanachuoni na watu wa Dini, kama alivyosema Shayk-ul-Islaam hapa na si kama ulivosema Muhammad Hassaan na si kama alivomtakasa ndugu ´Aliy Hassan bin ´Abdil-Hamiyd.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=EJOwM3UM4z4
  • Imechapishwa: 09/11/2014