Kunaogezewa juu ya hayo mapokezi kutoka kwa Maswahabah wakubwa. Wa kwanza ni Abu Bakr as-Swiddiyq na wa mwisho wao kiumri ni ´Abdullaah bin ´Umar bin al-Khattwaab (Rahimahu Allaahu ´anhum). Wote wamesema kuwa mwenye kuwahi Rukuu´ ameiwahi Rakaa´ hiyo. Hapa yameafikiana mapokezi kutoka kwa Salaf ambayo ni Swahiyh pamoja na Hadiyth hii Swahiyh. Kwa hivyo imethibiti ya kwamba yale maoni ya jamhuri ndio yenye nguvu.

Lakini mpaka hii leo kuna watu waliozama kidogo katika elimu ya Hadiyth wenye kuonelea kuwa mtu ambaye amewahi Rakaa´ hakuiwahi Rakaa´ hiyo. Nakumbuka kuwa Ghumaariy – hata kama ni katika Ahl-ul-Ahwaa´ na Suufiyyah ambao wana maneno yaliyopinda kutokamana na Sunnah – ameandika kijitabu ambapo ndani yake ametilia nguvu kuwa yule mwenye kuwahi Rukuu´ hakuiwahi Rakaa´ hiyo. Ana maoni mamoja kama baadhi ya Ahl-ul-Bid´ah waliyoko India.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (32)
  • Imechapishwa: 14/01/2017