al-Fawzaan watu wengi wakakusanyika na kusoma ndani ya maji

Swali: Je, inafaa nikiwa na maji na nikataka kuyasomea? Inafaa vilevile kutenga mtu zaidi ya mmoja wakayasomea?

Jibu: Kipingamizi kiko wapi? Kusoma ndani ya maji ni jambo limepokelewa katika Sunnah; mtu akayasomea maji na akapewa nayo yule mgonjwa. Ni jambo limepokelewa katika Sunnah. Kusoma ndani ya maji kwa sababu ya matabano hakuna neno. Inajuzu wewe na wale waliohudhuria wakasoma ndani ya maji. Hii ni aina moja wapo ya kujitibu kwa matabano.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (09) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/09.mp3
  • Imechapishwa: 06/04/2019