Jambo la pili, alilosema muulizaji kuhusu mambo ya watu haw

 

Swali: سماحة اشىخ [Samaahah ni msemo wa adabu], baadhi ya wasomaji wamefanya kazi ya Ruqyah ni kazi rasmi na wamefanya sehemu ya wanaume na wanawake. Je,kitendo hichi kinajuzu kwa kuwa kumewekwa sanduka ambapo kunawekwa pesa ndani yake?

Jibu: Mmekwishasikia maneno yangu kuhusu hili. Jambo la kwanza, msemo wenu kuwa mimi ni Samaahah, mimi sio mtu mwenye kustahiki hivyo. Mimi ni mtu masikini, mimi sistahiki hilo neno Samaahah na wala sio mtu wa fadhila. Nataraji mtaacha matamshi kama haya.

Jambo la pili, alilosema muulizaji kuhusu mambo ya watu hawa, ndo yale tulosema. Wanafanya mahali pa wanaume na wanawake. Haya ndio yale ya mwanaume kumtibu mwanamke… na ndugu yetu huu (muulizaji) kagusia jambo muhimu. Nalo ni mwanaume kumtibu mwanamke, kuchanganyika nae na kumgusa kwa madai kwamba anamsomea Ruqyah. Mambo yote haya ni vikwazo vya Kishari´ah. Jambo hili halijuzu. Akamtibu mwanamke, akamgusa au akachukua (akamfunua) kitu katika mwili wake ambacho ni wajibu kwake kukisitiri kwa madai ya kwamba anamsomea. Hili ni jambo lisolojuzu. Amsomee Mahram wake, au yeye mwenyewe ajisomee. Ni Muislamu wakike. Ajisomee mwenyewe au Mahram wake amsomee. Usiende kwa mwanaume ajinabi [awezae kukuoa] au mwanaume ambaye haaminiki kwa Dini yake na heshima yake. Tunamuomba Allaah Awaongoze Waislamu. Jambo hili inatakiwa kulitanabahi. Wanawake wanawaendea watu hawa na wanachanganyika nao. Kunatokea ufisadi na machafu kwa sababu ya jambo hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=r10tPkI2D4o
  • Imechapishwa: 26/03/2018