Swali: Wizara ya Kiislamu imeamua kwamba maimamu na makhatwiyb watahadharishe Jamaa´at-ut-Tabliygh. Pamoja na hivyo maimamu na makhatwiyb hawatahadharishi nao. Ni ipi hukumu ya hilo na ni ipi hukumu ya Jamaa´at-ut-Tabliygh?

Jibu: Ikiwa kuna walinganizi hawatahadharishi nao na hawatekelezi amri, mtu arejee katika wizara kuhusiana na mtu huyu na kuwaambia kuwa mtu huyu hakutekeleza amri. Baada ya hapo wizara itamchukulia hatua kwa njia munasibu.

Jamaa´at-ut-Tabliygh na wengine wote wanaoenda kinyume na mfumo wa Salaf-us-Swaalih wako katika makosa. Ima ni upotevu au ni kosa tu. Kwa hali yoyote njia iko wazi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia za vichochoro vitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo alivyokuusieni kwayo mpate kucha.” (06:153)

Yule mwenye kuacha njia na mfumo huu ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake walipita juu yake, ni katika mapote potevu ambayo Allaah Alitahadharisha:

وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“Na wala msifuate njia za vichochoro vitakufarikisheni na njia Yake.”

Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposifia kundi Lililookoka, wakauliza ni ipi. Akasema:

“Ni lile linalofuata yale niliyomo mimi hivi leo na Maswahabah zangu.”

Yanayoenda kinyume na yale aliyokuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake ameangamia na hakuokolewa. Haki iko wazi na mfumo uko wazi.

Sisi hatumfuati fulani na fulani. Tunamfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Allaah (Jalla wa ´Ala) Amesema:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

”Wale waliotangulia mwanzoni [katika Uislamu] katika Muhaajiriyn na Answaar na wale waliowafuata kwa wema; Allaah ameridhika nao, nao wameridhika Naye.” (09:100)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/allmohadrat?page=1
  • Imechapishwa: 23/04/2015