al-Fawzaan kuhusu uwalii wa mwanaume asiyeswali


Swali: Je, imeshurutishwa walii wa mwanamke atakayemuozesha awe amehifadhi swalah pamoja na mkusanyiko msikitini?

Jibu: Ndio. Ikiwa anaswali lakini haswali pamoja na mkusanyiko msikitni, huyu ni muasi na usimamizi wake haumtoki. Ama ikiwa haswali kabisa hata baadhi ya swalah, anaacha swalah kwa kukusudia, huyu ni kafiri na hapaswi kuwa walii wa Muislamu. Ni lazima awe na walii mwingine katika waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12934
  • Imechapishwa: 20/09/2020