Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya ´Umrah katika mwezi wa Rajab?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana. Lakini wanachuoni wengi wanaonelea kuwa haikuwekwa katika Shari´ah na kwamba hakukuwekwa kitu maalum katika Rajab. Ni mamoja ´Umrah au kitu kingine. Ni jambo halikuthibiti. Lakini kuna wanachuoni wanaosema kuwaf ´Umrah katika Rajab imependekezwa kwa sababu Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alikuwa akifanya hivo. Kwa hiyo wanapendekeza ´Umrah tu katika Rajab. Maoni haya yanahitajia kuangaliwa vizuri. Wanachuoni wengi wanaonelea kinyume na hivo na kwamba hakukuwekwa kitendo chochote maalum katika Rajab kwa kukosekana dalili juu ya hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/14590
  • Imechapishwa: 31/03/2018