al-Fawzaan kuhusu ujinga ni udhuru 8

Swali: Mama yangu amefariki hali ya kuwa ni mwenye kufungamana na mawalii hali ya kuwa anawatukuza na anawawekea nadhiri. Lakini hata hivyo ni mjinga ambaye hakusoma. Nilijaribu kumnasihi mara nyingi ili aachane na shirki lakini haikufua dafu. Amekwishafariki na mimi simtakii rehema, simuombei du´aa wala simuombei msamaha. Je, matendo yangu haya ni sawa?

Jibu: Ndio. Kwa sababu alikufa juu ya shirki:

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ

“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni.” (09:113)