al-Fawzaan kuhusu ujinga ni udhuru 7


Swali: Ambaye anatamka shahaadah lakini pamoja na hivyo anayaabudu makaburi na anayachinjia kwa sababu ya ujinga. Je, anatoka kwa kitendo chake hichi katika Uislamu?

Jibu: Hapewi udhuru kwa ujinga. Da´wah imefika. Ambaye amefikiwa na Da´wah hapewi udhuru kwa ujinga. Da´wah imefika ulimwenguni kote. Haifichikani kabisa. Isipokuwa yule ambaye ametika na ulimwengu na hafikiwi na kitu, hasikii adhana, swalah wala kitu chochote. Huyu anazingatiwa ni katika Ahl-ul-Fatrah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (92) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20%D9%85%D9%86%20%D9%85%D8%B5%D8%A7%D8%A6%D8%AF%20%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%8A%D8%B7%D8%A7%D9%86-29-07-1439%D9%87%D9%80%200010.mp3
  • Imechapishwa: 20/07/2018