Swali: Je, anapewa udhuru yule anayetumbukia katika vitenguzi hivi kwa ujinga?

Jibu: Ujinga unatofautiana. Ikiwa mjinga huyu hawezi kujifunza basi anapewa udhuru mpaka pale atapopata mtu wa kumfunza. Ni kama mfano wa yule ambaye anaishi na hana mawasiliano kabisa na miji ya waislamu. Katika mji huo hakuna isipokuwa makafiri tu. Huyu anapewa udhuru kwa ujinga.

Kuhusu yule ambaye anaishi kati ya waislamu na katika mji wa kiislamu ambapo anasikiia Qur-aan, anasikia Hadiyth na anasikia maneno ya wanachuoni. Huyu hapewi udhuru kwa ujinga kwa sababu imemfikia hoja. Lakini hata hivyo hakuitilia umuhimu. Bali huenda akasema: “Hii ni dhini ya Wahhaabiyyah”, “Hii ni dini ya watu wa Saudi Arabia” au ni dini ya fulani na fulani. Hivo ndivo wanavosema hii leo kuhusu Tawhiyd. Wanasema Tawhiyd ni dini ya Ibn ´Abdil-Wahhaab. Pamoja na kuwa Tawhiyd ndio dini ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ibn ´Abdil-Wahhaab hakuja na kitu. Hakuna alichofanya isipokuwa kulingania katika dini ya Mtume Ibn ´Abdil-Wahhaab. Matokeo yake wakamnasibishia dini kwake na kusema kwamba hii ni dini ya Wahhaabiyyah na kwamba ni dini ya Ibn ´Abdil-Wahhaab. Kuna wengine wanasema kuwa ni dini ya Khawaarij. Je, watu kama hawa wanastahiki kupewa udhuru? Watu hawa ni wenye jeuri na hawapewi udhuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 11/05/2018