al-Fawzaan kuhusu ujinga ni udhuru 4

Swali: Kuna maswali mengi yenye kuuliza masuala ya kupewa udhuru kwa ajili ya ujinga katika mlango wa ´Aqiydah ikiwa ni pamoja na swali hili lenye kusema kuwa mtu akikulia katika mji ambapo wanachuoni wake ni waabudu makaburi na mtu huyu amechukua elimu kutoka kwao kwa kutekeleza Kauli Yake (Ta´ala):

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Basi ulizeni watu wenye Ukumbusho ikiwa hamjui.” (16:43)

Jibu: Ndugu! Tawhiyd inaenezwa na kusambazwa leo kwenye vitabu na inaenezwa kwenye TV na njia za mawasiliano usiku na mchana. Wewe unasema kuwa wanachuoni wako ni makhurafi, ina maana hakuna wengine zaidi ya wanachuoni wako? Kuna wanachuoni wa Sunnah na wa Tawhiyd. Ni kwa nini anachukua maneno ya wanachuoni wake na anaacha ya wengine? Huyu ni mshabiki. Hapewi udhuru kwa ujinga. Kwa sababu hili limembainikia na kumfikia.Je, mtu huyu anakuwa ni mwenye kupewa udhuru?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Madjîd (25) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20-%2027-%2012-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017