al-Fawzaan kuhusu ujinga ni udhuru 3

Swali: Waabudu makaburi ni wajinga na hivyo hawakufurishwi kwa ajili hiyo?

Jibu: Mpaka lini watakuwa wajinga ilihali wanaishi kati ya waislamu, wanasikia Qur-aan, maneno ya wanachuoni na Hadiyth? Mpaka lini? Hoja imewafikia. Maadamu hoja imewafikia hawana udhuru wowote:

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ

“Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.” (06:19)

Mwenye kufikiwa na Qur-aan hana hoja yoyote. Wengi wao watu hawa wamehifadhi Qur-aan. Wamefikiwa na Qur-aan ambayo inakataza shirki, inatahadharisha shirki na inawakemea washirikina.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathulmajid%207%20-%20… Toleo la: 22.05.2015
  • Imechapishwa: 11/02/2017