al-Fawzaan kuhusu ujinga ni udhuru 13

Swali: Ikiwa mtu anaishi katika mji wa Kiislamu ambapo watu wengi wamefungamana na watu wema na hakuna wanachuoni wa Tawhiyd. Mtu huyu anawaomba watu hao wema na kujikurubisha kwao kwa kuwafanyia aina mbali mbali za ´ibaadah. Je, tumhukumu kufuru kwa dhati yake na kutangamana naye matangamano ya makafiri bila ya kumsimamishia hoja? Tunaomba utupambanulie.

Jibu: Ikiwa amefikiwa na Qur-aan na anaielewa basi anaingia katika kanuni niliyowatajia. Akifikiwa na Qur-aan na yeye ni mwarabu na anafahamu lugha ya kiarabu, basi amesimamikiwa na hoja.

Shirki ni kitu kiko wazi kabisa katika Qur-aan. Makatazo juu ya shirki ni miongoni mwa mambo yaliyo wazi kabisa katika Qur-aan. Sehemu nyingi imekatazwa, kutolewa makemeo na kutahadharisha juu yake. Hana udhuru. Ikiwa anaomba asiyekuwa Allaah ni mshirikina kwa dhati yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2137
  • Imechapishwa: 09/07/2020