al-Fawzaan kuhusu Tawhiyd al-Mutaaba´ah

Swali: Shaykh Hammaad al-Answaariy (Rahimahu Allaah) ametaja katika kitabu chake “Masaa-il fiyl-´Aqiydah” katika tafsiri ya “al-Faatihah” ya kwamba Tawhiyd ni vigawanyo vine ambapo akataja ya kwamba kigawanyo cha nne ni “Tawhiyd-ul-Mutaaba´ah” bi maana kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Ndio, kuna baadhi yao wamesema kuwa kuna kigawanyo cha nne. Lakini uhakika wa mambo sio katika Tawhiyd. Ni katika kufuata, al-Ittibaa´ na kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haisemwi kuwa ni Tawhiyd. Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah kwa ´ibaadah. Je, kunaweza kusemwa ya kwamba mwenye kwenda kinyume na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakuwa mshirikina? Mwenye kwenda kinyume na Tawhiyd anakuwa mshirikina tofauti na mwenye kwenda kinyume na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtu huyu anakuwa ni mtenda dhambi. Shaykh Hammaad amefuata maoni ya baadhi yao [wanachuoni]. Lakini hata hivyo yanahitajia kuangaliwa vizuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (36) http://alfawzan.af.org.sa/node/2133
  • Imechapishwa: 13/07/2020