Yule ambaye anapindisha na kusema kuwa Malaika ni maana tu na sio viwiliwili na kwamba ni zile hizia zinazomjia mtu. Hisia hizo zikiwa nzuri basi huyo ni Malaika na hisia hizo zikiwa mbaya basi huyo ni shaytwaan. Haya ni maneno ya kikafiri.

Kwa masikitiko makubwa yako katika “Tafsiyr-ul-Manaar” ambayo yamenukuliwa na Muhammad Rashiyd Ridhwaa kutoka kwa Shaykh wake Muhammad ´Abduh. Haya ni maneno ya wanafalsafa. Ni maneno batili. Mwenye kuyaamini ni kafiri. Lakini tunataraji kuwa aliyanukuu pasi na kuyaamini. Lakini kule kuyanakili bila kuyakosoa kuna khatari. Maneno haya ni batili na ni kuwakufuru Malaika. Tunamuomba Allaah afya na usalama.

Haitakiwi kwa mtu kuingiza akili na fikira zake au akanukuu kutoka kwa wanafalsafa au mazanadiki chochote katika mambo ya dini au mambo yaliyofichikana. Anachotakiwa ni kunakili kutoka katika Qur-aan na Sunnah, ndio jambo la wajibu.

Katika “Tafsiyr-ul-Manaar” imetajwa kwamba imenukuliwa kutoka katika “Ihyaa´ ´Uluum-id-Diyn” cha al-Ghazaaliy. Allaah ndiye anajua zaidi. Kitabu “Ihyaa´ ´Uluum-id-Diyn” cha al-Ghazaaliy ndani yake mna majanga na mabalaa ingawa ndani yake kuna kitu katika kheri na faida. Lakini ndani yake mna maangamizi na sumu kiwango kikubwa. Ni kitabu kilichochanganya mambo. Shari zake ni nyingi kuliko kheri zake. Kwa hivyo haipasi kwa yule mwanafunzi anayeanza au mtu wa kawaida kukisoma isipokuwa akiwa na elimu na uwezo wa kupambanua kati ya haki na batili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 211-213
  • Imechapishwa: 14/03/2020