al-Fawzaan Kuhusu tafsiri ya Aayah “Hakuna kulazimishana katika dini”

Swali: Vipi kujumuisha baina ya Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ

“Hapana kulazimisha katika (kuingia) Dini.” (02:256)

na baina ya kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nimeamrishwa kupigana vita na watu mpaka washuhudie “hapana mola mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah”?

Jibu: Huku sio kulazimisha. Nimeamrishwa kupigana vita na watu mpaka washuhudie “hapana mola mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah”, huku sio kulazimisha. Ama kuhusu Kauli:

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ

“Hapana kulazimisha katika (kuingia) Dini.” (02:256)

Imesemekana kwamba ni maalum kwa Ahl-ul-Kitaab. Imesemekana vilevile kuwa hili lilikuwa mwanzoni kisha baadaye likafutwa kwa kuwekwa Jihaad. Kauli sahihi – na Allaah ndiye Anajua zaidi:

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ

“Hapana kulazimisha katika (kuingia) Dini.” (02:256)

maana yake ni kwamba huwezi kumlazimisha yeyote kuingia katika Uislamu. Uongofu uko Mikononi mwa Allaah. Uongofu haumiliki yeyote isipokuwa Allaah. Huwezi kumlazimisha yeyote ukafanya moyo wake ukawa na uongofu. Unachoweza ni kumpiga vita, kumlingania katika Dini ya Allaah na kadhalika. Ama kusema uingize Imani ndani ya moyo wake, hili halimiki yeyote isipokuwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (48) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-04-15.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014