Swali: Ni yapi maoni yako juu ya kitabu “Tawassul ilaa haqiyqat-it-Tawasssul” cha Shaykh Muhammad ar-Rifaa´iy?

Jibu: Mimi sijakisoma. Lakini mtu huyu anajulikana kuwa ni Salafiy na ana ´Aqiydah nzuri. Ama kama kutakuwa kuna baadhi ya makosa sijui kwa kuwa sijakisoma. Lakini kuhusiana na mtu huyu ni mtu mzuri na ni miongoni mwa walinganizi wa Tawhiyd huko Shaam. Allaah amrehemu. Mara nyingi vitabu vyake ni vyenye kufidisha kutoka katika vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kwa kuwa mtu huyu anampenda sana Shaykh-ul-Islaam.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2104
  • Imechapishwa: 28/06/2020