Swali: Je, inajuzu kutoa nywele za kwenye kifua, mapaja na kwenye miguu au ni kujifananisha na wanawake?

Jibu: Hili mlilisoma jana katika Hadiyth ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiufanya mwili wake unang´aa. Kutoa nywele za mwilini ni jambo lisilokuwa na ubaya. Lililokatazwa ni kutoa ndevu na mwanamke kutoa nyusi zake. Haya ndio yamekatazwa. Ama kutoa nywele ambazo zinamuudhi mtu na zinakusanya harufu mbaya kwenye mwili wake na zinakuwa ndefu sana, hizi hakuna neno. Hili ni katika usafi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-6-9.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014