al-Fawzaan kuhusu muislamu kujilipua kati ya makafiri


Swali: Wakati wa vita baina ya Waislamu na makafiri inajuzu kuingia sehemu ya makafiri na mtu akajilipua?

Jibu: Hapana. Hapana. Kujiua? Hapana. Hapana. Asiue nafsi yake. Lakini anachoweza kufanya ni kuingia katika khatari, sawa ikiwa atasalimika au hatosalimika. Hakuiua nafsi yake, lakini ameuawa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema:

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا

”Na wala usiwadhanie kabisa wale ambao wameuawa katika njia ya Allaah ni wafu.” (03:169)

Hakusema:

”Na wala usiwadhanie kabisa wale ambao wamejizua katika njia ya Allaah ni wafu.”

Zingatieni Aayaat.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (58) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13521
  • Imechapishwa: 16/11/2014