al-Fawzaan kuhusu Mtume kuhudhuria maulidini

Swali: Baadhi ya Suufiyyah wanatumia dalili kwa Hadiyth:

“Niswalieni, kwani swalah [du´aa] zenu zinanifikia popote mlipo.”

Vilevile:

“Hakuna mja anayeniswalia isipokuwa Allaah hunirudishia roho yangu nikamrudishia.”

ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anahudhuria kwenye Maulidi yao au kwenye mikutano yao…

Jibu: Iko wapi dalili juu ya haya? Kwanza Maulidi yenyewe iko wapi dalili yenye kuonesha kuwa yemewekwa katika Shari´ah?

Pili ikiwa watatuletea dalili ya kwamba Maulidi yamewekwa katika Shari´ah, iko wapi dalili ya kuwa Mtume anahudhuria? Maiti hawatoki na wala hawarudi duniani. Hili ni sawa kwa Mitume na watu wengine. Mwenye kufa amesafiri kutoka duniani na wala hawezi kurudi duniani. Hakukuthibiti ya kwamba wanarudi na wanatembea juu ya ardhi na kadhalika:

أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ الْقُرُونِ أَنَّهُمْ إِلَيْهِمْ لَا يَرْجِعُونَ وَإِن كُلٌّ لَّمَّا جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ

“Je, hawajaona karne ngapi Tumeangamiza kabla yao hawazingatii kwamba wao hawatorejea kwao? Hapana yeyote ila wote watahudhurishwa Kwetu.” (36:31-32)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (36) http://alfawzan.af.org.sa/node/2133
  • Imechapishwa: 13/07/2020