al-Fawzaan Kuhusu Mfungaji Kufanya Jimaa Kwa Kusahau


Ni ipi hukumu ya kula, kunywa au kufanya jimaa kwa kusahau katika Swawm ya Naafilah?

Jibu: Mwenye kusahau Swawm yake haiharibiki, sawa ikiwa ni Swawm ya Naafilah au faradhi. Mwenye kusahau hachukuliwi wala Swawm yake haivunjiki. Haya yanahusiana na kula na kunywa. Kwa kuwa haya ndio yaliyothibiti.

Ama kuhusu kufanya jimaa haikuthibiti kwamba inaweza kuwa kwa kusahau. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuja yule mtu ambaye alimwambia kuwa amemwingilia mke wake ilihali amefunga, hakumwambia “Vipi, ulikuwa umesahau?” Hapana. Alimtolea Fatwa ya kutoa kafara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-03-14.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014