Swali: Uingereza tuna mbwa zilizofunzwa zinazowaongoza na kuwasaidia watu vipofu. Nina msichana kipofu aliye na miaka kumi na mbili. Hana mtu mwingine anayeweza kumsaidia siku zote na wakati huo huo ana haja kubwa ya kutoka kwa ajili ya mambo yake mbalimbali ya maisha yake. Inafaa kuwa na mbwa nyumbani kwa ajili ya jambo hili?

Jibu: Hapana. Haijuzu kuwa na mbwa kwa ajili ya kitu kingine isipokuwa yale mambo yaliyothibiti kwa dalili; mbwa kwa ajili ya mifugo, mbwa ya ulinzi na mbwa ya mawindo. Ni katika hali hizi tatu. Nyinginezo hapana. Hatuzidishi juu ya dalili kutoka kwetu wenyewe. Mbwa ni najisi. Mate na ngozi yake ni najisi. Malaika hawaingii ndani ya nyumba ilio na mbwa au picha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 03/11/2016