Yuusuf al-Qaradhwaawiy:

“Enyi ndugu! Kabla ya kuacha sehemu hii, nataka kusema neno kuhusu matukio ya uchaguzi wa Israaiyl. Waarabu walikuwa wameweka matumaini yao yote kwa ushindi wa Barleen, hata hivyo Barleen imeshindwa. Na hili tunaisifia Israaiyl. Twatamani nchi yetu ingekuwa kama nchi hii (Israaiyl). Kwa ajili ya mjumuiko mdogo wa watu wenyewe ndo wanahukumu (serikali). Hakuna asilimia 94% au asilimia 95% (ya uchaguzi) tofauti na tunavyojua katika miji yetu, asilimia 99% kwa asilimia 100%. Mambo gani haya?! Lau hata Allaah Mwenyewe Angehudhuria kwa watu asingelipata kiasi chote hiki cha kura kutoka kwa watu… Huu ni uongo, udanganyifu na hadaa. Tunaikaribisha Israaiyl kwa ilichofanya.”

Swali: Kuna mtu miongoni mwa wale wanaojinasibisha na elimu na anaonekana mara nyingi kwenye TV amesema:

“Kwanza anawasifu Israaiyl upande wa uchaguzi na msemaji huyu ametamani utaratibu wa uchaguzi uliopitika Israaiyl uwepo katika miji ya kiarabu na kwamba mmoja katika wagombezi alipata 99%. Mtu huyu akaweka taaliki na kusema: “Lau Allaah mwenyewe angelijionyesha kwa viumbe Wake basi asingelipata asilimia yote hii.” Ni yepi maoni yako?

Jibu: Haya ni maneno yasiyokuwa na maana na yenye kupitiliza. Ni kuwa na utovu wa adabu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hii ni dalili inayoonyesha kuwa mtu huyu hana akili na hana maana yoyote. Ni wajibu kwake kutubu kwa Allaah na aache mfano wa maneno mabaya kama haya.

Waislamu – na himdi zote zinamstahikia Allaah – wako katika kheri. Waislamu wako katika kheri. Mayahudi vovyote watavofanya basi itambulike kuwa wao ni manyani na nguruwe. Hawana kheri yoyote. Haijalishi yale watayofanya. Wao ni maadui wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Kuhusu waislamu, hata kama kutatokea kwao mapungufu na kasoro, ndani yao kuna kheri nyingi na himdi zote zinamstahikia Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 14/11/2017