al-Fawzaan kuhusu kutumia Injiyl na Tawrat katika kujadiliana na makafiri

Swali: Je, inajuzu kutumia kama dalili Injiyl na Tawrat ambavyo kwa hivi sasa viko kwenye mikono ya manaswara na mayahudi kwa yale yanayoafikiana na Shari´ah yetu?

Jibu: Shari´ah yetu inatosheleza na himdi zote ni Zake Allaah. Shari´ah yetu inatosheleza na haina upungufu. Imekamilika.

Lakini kutumia kama dalili Tawrat na Injiyl kwa ajili ya kuwasimamishia hoja juu yao na kujadiliana nao, hakuna neno kufanya hivo kwa yule anayejua hili kwa wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-15.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014