al-Fawzaan kuhusu kunywa sumu kwa Khaalid bin al-Waliyd

Swali: Yaliyopokelewa kuwa Khaalid bin al-Waliyd (Radhiya Allaahu ´anh) alikunywa sumu na haikumdhuru ni moja katika karama?

Jibu: Ndio, bila ya shaka. Hii ni katika karama. Khaalid bin al-Waliyd alifanya kitu kisichokuwa cha kawaida. Khaalid bin al-Waliyd ni Swahabah mtukufu, mpambanaji na ni kiongozi ambaye alikuwa ni shujaa ambaye alikuwa akipigana Jihaad katika njia ya Allaah. Mambo yasiyokuwa ya kawaida yenye kupitika kwake inakuwa ni katika karama. Hili halina shaka yoyote.

Alifanya hivi kwa sababu ya kusimamisha hoja katika dini kama tulivyotangulia kuwaambia. Lengo ilikuwa kusimamisha hoja katika dini ili adhihirishe kuwa dini hii ni haki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (13) http://alfawzan.af.org.sa/node/2128
  • Imechapishwa: 05/07/2020