al-Fawzaan kuhusu kumuozesha bikira kwa nguvu


Swali: Je, inajuzu kwa baba kumlazimisha msichana wake ambaye ni bikira kuolewa? Nimesoma masuala haya kwenye kitabu kimoja.

Jibu: Hakuna ulazimishaji. Asimlazimishe msichana wake kuolewa, sawa ikiwa ni bikira au kishawahi kuolewa. Bikira inatakiwa ichukuliwe rai yake na wala asiozeshwe na yule anayemchukia, maadamu yuko na akili na anajua maslahi yake. Asilazimishwe kutokana na kauli sahihi miongoni mwa kauli za wanachuoni. Kama ilivyokuja katika Hadiyth ya kwamba bikira atakwe idhini na kutoa kwake idhini ni kule kunyamaza kwake kimya. Mama mzima ambaye kishawahi kuolewe aamrishwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12934
  • Imechapishwa: 20/09/2020