al-Fawzaan kuhusu kumpa mtoto jina la Hudaa na Iymaan

Swali: Je, inajuzu kuitwa kwa jina la Hudaa?

al-Fawzaan: Kumpa nalo mtoto wa kiume au wa kike?

Muulizaji: Wa kike.

Jibu: Hakuna neno. Kuitwa kwa jina la Hudaa hakuna neno. Lililokatazwa ni kuitwa kwa jina la Dhwalaal au Kufr na kadhalika. Ama kuitwa kwa jina la Hudaa, Iymaan na kadhalika, hili ni jambo zuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-5-25.mp3