al-Fawzaan kuhusu kufunga mchana au usiku wa tarehe 15 Sha´baan

Swali: Je, kumepokelewa Hadiyth kuhusu nusu ya Sha´baan? Je, imepokelewa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunga mwezi mzima?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga siku nyingi za Sha´baan. Bi maana alifunga masiku yake mengi.

Kuhusu kukhusisha usiku au mchana wa nusu ya Sha´baan ni jambo halina dalili. Hakukusihi dalili juu ya hilo. Hadiyth zote zilizopokelewa juu ya hilo si Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1436-03-02.mp3
  • Imechapishwa: 02/12/2017