Swali: Ni yapi maoni yako juu ya kitabu “as-Suufiyyah” cha Muhammad ´Abduh na kitabu “Haadhihiy as-Suufiyyah” cha ´Abdur-Rahmaan Wakiyl?

Jibu: Kuhusu kitabu “as-Suufiyyah” cha Muhammad ´Abduh mimi sijakiona. Sijui anakusudia Muhammad ´Abduh yupi; ni yule ambaye alikuwa Mufty wa Misri katika wakati wake au ni Muhammad ´Abduh mwingine. Allaah ndiye anajua zaidi. Mimi sijaona kitabu hichi.

Kuhusu kitabu cha ´Abdur-Rahmaan Wakiyl ni kitabu kizuri. Yeye ndiye amewaponda Suufiyyah, akawafedhehesha, akawafichukua na akabainisha aibu na upotevu wao. Ni kitabu kizuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (13) http://alfawzan.af.org.sa/node/2056
  • Imechapishwa: 02/04/2017