Swali: Ni sahihi kuwa radi ni sauti ya Malaika? Inajuzu kwa baba kumpa mwanae jina la “Ra´d”, radi?

Jibu: Ni sawa. Ampe jina analotaka midhali sio majina ya haramu. Haijuzu kwake kumpa majina ya haramu kama mfano wa ´Abdul-Husayn, ´Abdur-Rasuul na majina mengine yenye kuashiria ya kwamba mpewaji ni mja wa mwengine asiyekuwa Allaah. Haijuzu. Majina mengine yote yanajuzu. Lakini hata hivyo inatakiwa kwa baba amchagulie mwanae jina zuri, kwa kuwa jina linafahamisha ni nani yule mpewaji.

Kuhusiana na radi, Allaah ndiye anayejua uhakika wake. Hali kadhalika ule umeme unaowaka. Ni katika alama za Allaah:

هُوَ الَّذِي يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنشِئُ السَّحَابَالثِّقَالَ

“Yeye ndiye Anayekuonyesheni umeme khofu na matumaini na anaanzisha mawingu mazito.” (13:12)

Ni moja katika alama za Allaah (´Azza wa Jall). Kuhusu uhakika wake, huku ni kubahatisha tu. Baadhi wanasema kuwa ni mawingu yamegongana, wengine wanasema kuwa ni sauti ya Malaika na kadhalika. Allaah ndiye anajua zaidi. Lakini hata hivyo ni katika alama za Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340126_0.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020